Kunakaribia kukucha Brazil wakati dimba la dunia litakapong'oa nanga.
Lakini kwa mara nyingine swala ibuka wakati huu
sio jipya. Je ngono inaathiri au kuimarisha uwezo wa mchezaji kuingiza
mabao au kusakata kabumbu vyema uwanjani?
Kuna ushahidi finyu kuwa ngono
inaathiri kivyovyote uwezo wa mchezaji uwanjani,sasa je kwa nini dhana
hii haindoki vinywani mwa wengi ?
Mexico na Brazil zimewaonya wachezaji wao dhidi
ya kujihusisha na ngono kabla ya mchi zao. Wachezaji wa Bosnia
Herzegovina pia wameonywa kuwa mashangingi na makahaba na wapenzi
wengine hawakaribishwi kambini.
Lakini Marekani imekuwa huru kidogo, kwamba
wachezaji hawana vikwazo vyovyote. Mwaka 2010, timu ta Argentina ilikuwa
huru kujihusisha kingono walivyotaka wachezaji ila matokeo yalikuwa
duni kiasi cha kocha Diego Armando Maradona kufurushwa kama kocha wa
timu hiyo.
Kocha Sven aliwaruhusu wachezaji kama Beckham kuandamana na mkewe Brazil |
Tabia ya wachezaji kingono wakati wa michuano ya
kombe la dunia, imejulikana miaka nenda miaka rudi. Vyombo vya habari
vimekuwa vikibugia taarifa za kila aina kuhusiana na ngono na wachezaji
wakati wa michuano ya kimataifa kama hii.
Timu ya England mnamo
mwaka 2006 ilitajwa kama sarakasi baada ya meneja wa timu hiyo Sven
Goran Eriksson kuruhusu wake wa wachezaji David Beckham na Ashley Cole
kuambatana na waume wao.
Miaka minne baadaye Fabio Capello aliwaonya wachezaji dhidi ya kujihusisha na ngono wakati wa mechi nchini Afrika Kusini.
Inafahamika vyema miongoni mwa wataalamu wa
maswala ya michezo kuwa ngono haitahiri hali ya mchezo wa mchezaji bora
tu mchezaji aweze kupata leope la usingizi.
Lakini dhana hii ya ngono kuathiri wachezaji kabla ya mchezo haipo tu kwenye soka bali pia riadha.
Mwanariadha daima alikuwa akisema, Linford Christie kufanya tendo la ndoa kabla ya mashindano ilifanya miguu yake kulegea.
Naye
mchezaji tennis wa zamani Ujerumani Boris Becker naye aligonga vichwa
vya habari alipokwenda kinyume na agizo la kocha wake kwamba ajizuie na
ngono.
Kadhalika mwanamasumbwi Carl Froch alijizuia na
ngono kwa miezi mitatu kabla ya kumshinda George Groves katika shindano
lao la mimataifa.
Hoja hii bila shaka haitapata jibu leo ikiwa
kweli ngono huathiri uwezo wa mchezaji, mwandishi wa habari za michezo
Hunter Davies anadhani kuwa mjadala huu huwa ni gumzo tu ambalo watu
wanapenda kupiga.
0 comments:
Chapisha Maoni