Jumatano, Juni 25, 2014

KANDORO AWATAKA WALIOATHIRIKA NA MADAWA YA KULEVYA MBEYA WAKIMBILIE TIBA


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka wananchi walioathirika na dawa za kulevya kujitokeza kwa wingi kupima afya zao, kupata tiba na ushauri katika maadhimisho hayo.
Kandoro alifafanua kuwa maadhimisho hayo yanafanyika mkoani humo kutokana na takwimu kuonyesha una kiwango kikubwa cha tatizo la dawa za kulevya kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na kutoa mfano wa bangi ambayo inalimwa kwa wingi.
Kama mnavyojua, mkoa wetu upo mpakani hivyo tuna changamoto kubwa sana ya uingizaji wa dawa hizi, mara nyingi watu hukamatwa katika mipaka ya Tunduma na Kasumulo, hivyo ni budi elimu hii kutolewa kwa wananchi ili tushirikiane wote katika kutokomeza vita hii tuliyonayo
alisema Kandoro.
Alisema kuwa pombe aina ya viroba vya bei nafuu vitokavyo Malawi ni changamoto pia kwani vijana wengi wanavitumia, hivyo kuathirika kwa kiasi kikubwa.

0 comments:

Chapisha Maoni