Uruguay ilifunga bao la ushindi katika dakika za mwisho na kuwabandua washindi mara nne wa kombe la dunia Italia .
Hata hivyo habari kuu kutoka katika mechi hii ilikuwa ni kashfa nyingine ya tukio la Luiz Suarez ‘kung’ata’
Mshambulizi huyo wa Liverpool
alionekana kumng’ata beki wa Juventus Giorgio Chiellini dakika moja
kabla ya Diego Godin kufungia Uruguay bao la ushindi.
Mapema katika mechi hiyo, kiungo cha kati wa
Italia Claudio Marchisio alikuwa ameonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea
vibaya Egidio Arevalo.
Uruguay sasa itacheza dhidi ya Colombia au Ivory
Coast jijini Maracana siku ya Jumamosi katika raundi ya pili ya Kombe
la Dunia, lakini utata unatarajiwa kuibuka kabla ya siku hiyo.
Italia walitoka uwanjani wakiwa na ghadhabu
kutokana na waliyoshuhudia kabla yao kuondolewa katika kombe la Dunia
la pili bila kupita kutoka mechi za makundi- kwa mara ya kwanza tangu
mwaka wa 1966.
Kocha wa Italia Cesare Prendelli alisema kabla
ya mchezo kuwa ilikuwa “mechi muhimu sana katika taaluma yake kandanda”
na baada ya kushindwa akapendekeza kujiuzulu.
Mechi hii ilikuwa na hamaki na hasira ndani na nje ya uwanja.
Mara
kwa mara wasaididizi wa refari walilazimika kuzuia zogo kati ya timu
hizo mbili, kipenga cha refarii kikatiza mchezo mara nyingi na wachezaji
wakachukua muda mrefu wakisukumana walipokuwa wakikimbia na mpira
miguuni.
Italia ilikuwa ikihitaji sare tu ili kufuzu.
Katika mfumo wa 3-5-2, Italia walikosa mshikamano, mbio na walihatarisha
lango lao kila wakati. Lakini iwapo mfumo wao ulitekelezwa ili kuzuia
ushambulizi wa Uruguay, mfumo huo ulisaidia.
Andrea Pirlo alimlazimu mlindalango wa Uruguay
Fernando Muslera kuondoa mkwaju wake uliotokana na mpira wa adhabu na
kuugongesha mlingoti, huku mshambulizi Ciro Immobile akipiga mkwaju nje
ya lango.
Edinson Cavani alitaka kuzawadiwa mkwaju wa
penalti katika dakika ya 50 baada ya kuangushwa na Andrea Barzagli,
lakini refarii akapuuzilia mbali.
Refarii huyo raiya wa Mexico hata hivyo
angebadili mchezo muda mfupi baadae wakati alipomwonyesha Marchisio kadi
nyekundu baada ya kiungo huyo wa kati wa Juventus kumchezea vibaya
Arevalo katikati mwa uwanja.
Marchisio alinyanyua mguu na kumgonga kiungo huyo wa Uruguay gotini.
Suarez alikaribia kufunga bao alipopiga mkwaju wa chini kwa chini ambao Buffon aliudaka .
Utata zaidi ulizuka wakati Suarez na Chiellini
walipokumbana katika maeneo ya penalti zikiwa zimesalia dakika tisa kwa
mechi kukamilika.
Beki huyo wa Italia alilalamika wakati huo huo kwa refarii kwamba alikuwa ameng’atwa na akajaribu kumwonyesha alama.
Wakati wachezaji wa Italia walipokuwa wakiendelea kulalamika, Uruguay wakapata kona.
Suarez alipiga pasi nzuri naye Godin akafunga bao hilo la ushindi.
Itali walijaribu kila wawezalo ili kupata bao,
hadi mlindalango Buffon kujaribu kutafuta bao kutokana na kona
waliyopata waitaliano dakika za mwisho, lakini upande wake Oscar Tabarez
ukawadhibiti.
Hata hivyo huenda mechi hii isikumbukwe sana. Macho yote, kwa mara nyingine yatamwelekea Suarez.
0 comments:
Chapisha Maoni