WAKIWA na uhakika wa kuongoza Kundi C, Colombia walifanya kitu cha
kuwafanya kuweka rekodi kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea
kupamba moto nchini Brazil.
Colombia ilifanya mabadiliko kwa kumwingiza kipa, Faryd Mondragon na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kucheza kwenye Kombe la Dunia.
Kipa huyo wakati anaingia uwanjani kudaka usiku wa kuamkia jana Jumatano alikuwa na umri wa miaka 43 na siku tatu na alicheza dhidi ya Japan kwenye mchezo ambao Colombia iliibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Hizo ni fainali za sita za Kombe la Dunia kwa Mondragon akiwahi pia kucheza mechi za kufuzu na kwamba alikuwa akianza golini sambamba na Oscar Cordoba kwenye fainali za Kombe la Dunia Marekani mwaka 1994.
Kwenye mchezo huo, Mondragon, aliingia uwanjani zikiwa zimebaki dakika tano tu na Colombia ilifanya hivyo ili kumpa kipa huyo nafasi ya kuweka rekodi kwenye fainali hizo.
Kocha wa Colombia, Jose Pekerman alifanya hivyo kutibua rekodi ya Roger Milla wa Cameroon, ambaye alikuwa akishilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa kucheza Kombe la Dunia kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Milla alikuwa akishikilia rekodi hiyo kwa kucheza akiwa na umri wa miaka 42, mwezi mmoja na siku nane wakati alipocheza fainali za Kombe la Dunia za Marekani mwaka 1994.
Kwenye miaka yake 24 kwenye soka, Mondragon aliwahi kuzichezea klabu ya Independiente na Galatasaray ya Uturuki.

0 comments:
Chapisha Maoni