Kombe la dunia Brazil 2014 linatarajiwa kungo'a nanga
baadaye leo jioni huku Brazil na Croatia wakitoana kijasho mjini Sao
Paolo.
Dimba hilo litakalodumu kwa mwezi mmoja,
litashuhudia mataifa 32 yakimenyana kuwania kombe hilo katika fainali
itakayochezwa mjini Rio tarehe 13 Julai.
Mechi ya ufunguzi itaanza baada ya
sherehe ya kufungua mechi hiyo mjini Sao Paulo. Ni mechi ambayo itakuwa
inatoa kipaombele kuonyesha umuhimu wa kukuza vipaji, utu na kabumbu.
wacheni niwambie kuwa wakati umewadia. Tunaenda sote . Hili ni kombe letu la dunia
alinukuliwa akisema kocha wa
Brazil Luis Felipe Scolari.
Mwaka jana zaidi ya watu milioni moja
walishiriki katika maandamano ya kupinga hatua ya serikali kuandaa
michezo hiyo kwa gharama ya juu wakati wananchi wengi wakiishi kwa
umasikini.
Serikali ya Brazil iko makini kuzuia kutokea
tena kwa ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano hayo. Rais Dilma
Rousseff amesema kuwa hatakubali kamwe maandamano yanayosababisha ghasia
kuathiri kombe la dunia.
Maelfu ya polisi na wanajeshi watashika doria nchini humo kuhakikisha kuwa mechi zinafanyika bila vurufu.
England itacheza mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Italy Jumamosi tarehe 14 , mechi ambayo itapeperushwa moja kwa moja na BBC.
Timu hiyo pia itacheza dhidi ya Uruguay na Costa Rica katika kundi D.
Wenyeji Brazil wataanza mechi leo wakipigiwa
upatu kushinda kombe la dunia kwa mara ya sita wakati mabingwa watetezi
Hispania nao wanakilenga kushinda kombe hilo kwa mara ya nne baada ya
kushinda ubingwa wa Ulaya miaka miwili iliyopita.
0 comments:
Chapisha Maoni