Mwandalizi mmoja wa mazishi nchini Afrika
Kusini,anayedaiwa kuwaagiza wafanyakazi wake kuikata miguu ya maiti moja
aliyodai kuwa ndefu sana alifikishwa mahakamani Ijumaa.
Ronel Mostert anayemiliki chumba cha kuhifadhi
maiti ambacho pia huendesha shughuli za mazishi, alitoa amri hiyo kwa
lengo la kuhakikisha kuwa maiti hiyo ingetosha katika jeneza.
Anakabiliwa na kosa la kumkata miguu maiti. Mfanyakazi mmoja aalimbia mahakama kuwa Ronel
alimuagiza kuchukua kifaa kimoja cha kukata ili kuikata miguu hiyo ya
marehemu na kwamba jambo hilo limekuwa likimsumbua sana kimawazo.
Mwili marehemu ulifukuliwa ili kusaidia katika uchunguzi wa polisi.
0 comments:
Chapisha Maoni