Jumatatu, Mei 19, 2014

USAFIRI WASITISHWA TAZARA-MBEYA KUTOKANA NA MGOMO

Shirika la reli Tanzania na Zambia (TAZARA) limesitisha za usafiri baada ya mgomo unaofikia siku ya tatu leo kufuatia wafanyakazi kutolipwa mishahara ya hadi miezi mitatu.
Akiongelea mgomo huo mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TAZARA kanda ya Mbeya, Christopher Kazia amesema kuwa uamuzi huo umetokana na wafanyakazi kutolipwa mishahara kwa kipindi cha miezi mitatu.Pamoja na hayo mwenyekiti Christopher amesema kuwa huduma zimesitishwa kwa muda ili kupisha vikao vya wafanya kazi kulijadili tatizo lao lakini pia ametoa lawama kwa uongozi kushindwa kuliendesha shirika hilo kiasi cha wakati mwingine kukosa hata mafuta kitu kinachosababisha uzalishaji mdogo.
Kwa upande wa abiria, bw. Bernad Giribat amesema kuwa mgomo huo umeathiri kwa kiasi kikubwa wasafiri kwani wamejikuta wakitumia gharama zaidi kwa upande wa malazi na cha chakula pamoja na ratiba zao kuvurugika huku wakitoa wito kwa shirika hilo kumaliza matatizo yao ili shughuli ziendelee kama kawaida.

0 comments:

Chapisha Maoni