Jumanne, Mei 13, 2014

TUNDU LISSU NA MUUNGANO TENA!!!

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Tundu Lissu aendelea kulilia serikali tatu, soma alichokiandika
Mzee Pius Msekwa, Mwenyekiti mstaafu wa CCM na Spika wa Bunge hili tukufu, aliwahi kusema katika mada yake Hali ya Muungano kwenye Semina Iliyofanyika Tanga miaka 20 Iliyopita kwamba "Muundo wa sasa wa Muungano huu, umepelekea wengi kuamini kwamba Muungano huu ni Kiini macho tu".............. Ni kweli kwamba Muungano huu ni wa Kipekee kwa Sababu haujawahi kuigwa na Nchi nyingine yoyote katika Afrika. Na kama Muungano huu ungekuwa wa Kupigiwa mfano Duniani kote kama Inavyodaiwa na Waziri Mkuu katika hotuba yake, basi kungekuwa na angalau Nchi moja Iliyoomba Kujiunga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aidha angalau baadhi ya Nchi za Afrika au Duniani kote zingeiga mfano wa Muungano huu. Kwa kuwa hakuna Nchi hata moja Iliyofanya hivyo, Mheshimiwa Spika pengine huu ni muda mwafaka wa kuhoji ukweli wa Kauli kwamba Muungano huu ni Kielelezo cha Umoja, Mshikamano na Upendo miongoni mwa Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar...................

0 comments:

Chapisha Maoni