Msemaji wa jeshi la serikali, Kanali Philip
Aguer, alisema wapiganaji wameshambulia maeneo ya serikali katika mji wa
Bentiu leo alfajiri.
Wapiganaji wamewashutumu wanajeshi wa serikali kuwa waliwashambulia katika sehemu kadha katika majimbo ya Upper Nile na Unity.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini
Ijumaa, na yalikusudiwa kumaliza vita vya miezi mitano ambavyo vimeuwa
maelfu ya watu na kulazimisha zaidi ya milioni moja kuhama makwao.




0 comments:
Chapisha Maoni