Waziri Mkuu wa Uchina, Li Keqiang, na viongozi wa
Afrika Mashariki wametia saini rasmi makubaliano ya kujenga njia mpya ya
reli itayounganisha mji wa Kenya wenye bandari, Mombasa, hadi Nairobi,
Rwanda na Sudan Kusini.
Waziri Mkuu wa Uchina yuko mjini Nairobi akiwa katika ziara ya Afrika.
Njia hiyo ya reli ya upana unaotumika kawaida
duniani itagharimu mabilioni ya dola, na itachukua nafasi ya njia ya
reli ya sasa ambayo ni nyembamba na ilijengwa zama za ukoloni wa
Uingereza.
Sehemu ya kwanza ya reli itajengwa na kampuni za
Uchina - jambo lilozusha malalamiko kwamba kampuni nyengine
hazikuruhusiwa kushiriki katika kuomba kandarasi.




0 comments:
Chapisha Maoni