Mlinzi kiraka wa timu ya Young Africans Mbuyu Junior Twite leo
ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu ya
Yanga baada ya kufikia makubaliano na uongozi na kupata majibu ya
Shirikisho la Soka nchini TFF juu ya idadi ya wachezaji wa kimataifa kwa
msimu ujao 2014/2015.
Usajili wa Twite umefanyika leo makao makuu ya klabu ya Yanga chini
ya Katibu Mkuu Bw Beno Njovu ambapo mchezaji amesema ataendelea
kujitolea kwa uwezo wake kuisaidia timu yake ya Yanga.
Katibu Mkuu
wa Young Africans Beno Njovu amesema wameingia mkataba wa mwaka mmoja
na Twite baada ya pande zote kukubaliana, hivyo kuanzia sasa Twite
ataendelea kuwa mchezaji wetu kwa msimu ujao wa 2014/2015 na kusisitiza
kuwa usajili ndio umeanza sasa.
Akiongea mara baada ya kuweka
sahihi kwenye mkataba wake mpya Twite amesema anajisikia furaha
kuendelea kuwa mchezaji wa Yanga, kwani anafurahia maisha ya Jangwani,
wapenzi, washabiki, viongozi na wachezaji ni marafiki/ndugu ndani na nje
ya Uwanja.
Aidha Twite amesema Yanga ni miongoni mwa timu kubwa
barani Afrika, zenye washabiki na waachama wengi hivyo wangu ni fahari
kuendelea kuitumika timu hii ambayo tangu kujiunga nayo nimekua nikijtoa
kwa moyo wangu wote kusaka mafanikio.
Mbuyu Twite amekua ni
mchezaji wa Young Africans kwa kipindi cha miaka miwili tangu Julai 2012
alposajiliwa huku katika kipindi hicho chote akiwa ni mchezaji wa
kikosi cha kwanza ambapo msimu uliopita aliweza kuisadia timu yake
kutwaa Ubingwa wa Lig Kuu ya Vodacom na msimu huu kushika nafasi ya
pili.
0 comments:
Chapisha Maoni