Alhamisi, Mei 22, 2014

KUMBE KABLA YA KIFO, AMINA NGALUMA ALIACHA WOSIA KWA ROSE MHANDO, SOMA HAPA

Wakati mwili wake ukipokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar, leo baada ya kukutwa na umauti nchini Thailand, imechimbuliwa kwamba siku chache zilizopita mwimbaji wa dansi Bongo, Amina Ngaluma ‘Japanese’ (41) alimwachia ujumbe staa wa Injili, Rose Muhando kabla ya kukutwa na umauti.
Mwanamuziki huyo wa siku nyingi ambaye alifariki dunia nchini humo baada ya kusumbuliwa na uvimbe kichwani, kabla ya kukutwa na umauti alionesha kushtushwa na video mpya ya wimbo wa Rose uitwao Mungu Anacheka.
Baada ya kutazama video hiyo alishangazwa na mavazi ya kubana aliyotumia Rose kwenye video hiyo.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Ngaluma alimkumbusha Rose kuwa ni mtumishi wa Mungu hivyo anapaswa kuangalia maadili hasa kwa video ya wimbo mzuri kama huo kwani itamjengea sura tofauti kwenye jamii.

Ngaluma aliomba kama kuna mtu wa Rose wa karibu amfikishie ujumbe wake huo.
Kifo cha Ngaluma kilitokea katika Hospitali ya Vanchira Phuket 83150 nchini Thailand ambapo ilisemekana kwamba alianza kusikia maumivu makali kichwani, uchunguzi ulipofanyika ikaonekana damu ilivilia kwenye ubongo.
Akizungumza kutoka Thailand, kiongozi wa bendi aliyokuwa akiitumikia Ngaluma, Hassan Shawu alisema mwanamuziki huyo alianza kuumwa Mei 11, mwaka huu na kupelekwa hospitali alikolazwa kabla ya kufariki Mei 15, mwaka huu ambapo msiba uliwekwa kwake, Kitunda-Machimbo, Dar.
Akizungumza na mwanahabari wetu nyumbani hapo, mume wa Ngaluma, Rashid Sumuni alisema alipokea simu  kutoka Thailand kuwa  mkewe aalikuwa anaumwa lakini hukuweza kufanya naye mawasiliano kutokana na hali aliyokuwa nayo.
Ngaluma aliwahi kuzitumikia bendi mbalimbali zikiwemo JKT Taarab, Sayari Band, Mangelepa, African Revolution ‘Tamutamu’, Double M Sound, TOT na  Jambo Survivors aliyokuwa akiitumikia hadi anakutwa na umauti.

0 comments:

Chapisha Maoni