Mapambano dhidi ya mbu wanaoeneza ugonjwa wa dengue na magonjwa
mengine yako mbioni kufanikiwa kutokana na kiwanda cha kuzalisha dawa ya
kuua mazalia yake kuanza uzalishaji mwezi ujao.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk
Stephen Kebwe alisema hayo bungeni jana alipokuwa akijibu maswali ya
wabunge kuhusu ugonjwa huo hasa gharama za upuliziaji dawa na vipimo na
sababu za kusambaza vyandarua badala ya kupambana na mbu.
Dk Kebwe ambaye awali alisema hadi sasa vyandarua
milioni 38 vimesambazwa nchi nzima na vingine milioni 6 vitasambawa
mwaka huu, alibainisha kuwa kiwanda hicho kinajengwa Kibaha mkoani Pwani
kwa ushirikiano na Serikali Cuba.
Akizungumza baadaye nje ya Bunge, Dk Kebwe alisema
kiwanda hicho kitaanza majaribio Juni mwaka huu na kuanza uzalishaji
rasmi Septemba.
Alisema dawa zitakazozalishwa katika kiwanda hicho
zitakuwa za kupuliza na zitatengezwa katika mfumo wa dawa jamii ya
Pyrethroid.
Dawa za aina mbalimbali zitazalishwa na zitakuwa na uwezo wa kuua mbu katika hatua zote tatu za ukuaji wake, kuanzia kwenye lava, viluilui na mbu wapevu
Kiwanda hicho kitakuwa kinazalisha dawa hizo na sisi tutazinunua kwa gharama nafuualisema.
Naibu waziri alibainisha kuwa kiwanda hicho huenda
kingekamilika mapema mwaka huu Juni 30, Serikali ilikuwa imetenga Sh3
bilioni kwa ajili ya kununua dawa hizo na vifaa vingine vya dharura.
Alifafanua kuwa kiwanda hicho kitainua uchumi wa
nchi na kuongeza ajira kwa wananchi kwa maelezo kuwa utengenezaji wake
hutegemea kwa kiasi kikubwa zao la pareto.
Awali ulitokea mvutano na maswali ya kila aina
bungeni kuhusu vipimo na jinsi ya kukabiliana na mbu wanaosambaza homa
ya dengue huku Serikali ikieleza kuwa tayari imeshasambaza vifaa vya
kupima homa hiyo nchi nzima.
Katika swali lake la nyongeza Mbunge wa Kinondoni
(CCM), Idd Azzan alihoji sababu za gharama za kupulizia dawa katika
magari ya abiria kuwa Sh65,000, huku akihoji nini mkakati wa Serikali
kuua mazalia ya mbu.
Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Nyamagana,
Ezekia Wenje alihoji sababu za Serikali kusambaza vyandarua badala ya
kuua mazalia ya mbu.
0 comments:
Chapisha Maoni