Kashfa imeikumba Hospitali ya Saratani ya Ocean Road (ORCI)
kutokana na tuhuma za mmoja wa wauguzi wake kumuuzia dawa ‘feki’ mgonjwa
ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika taasisi hiyo ya Serikali.
Mtumishi wa ORCI katika kitengo cha dawa, Almasi
Matola anatuhumiwa kudai fedha kwa mmoja wa wagonjwa wa satarani (jina
tunalihifadhi kwa sasa), lakini akampa dawa feki baada ya kupewa fedha.
Mgonjwa huyo alipewa rufaa kwenda Ocean Road
Novemba mwaka jana akitokea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya
kubainika kwamba alikuwa na saratani ya titi.
Baada ya kufika ORCI, ilibainika kwamba mgonjwa
huyo alikuwa akihitaji tiba ya kuua vijidudu vya saratani inayojulikana
kitaalamu kwa jina la chemotherapy au chemo kwa kifupi na ndipo
alipokutana na Matola.
0 comments:
Chapisha Maoni