Rais wa Malawi, Joyce Banda amesema udanganyifu mkubwa umetokea kwenye
uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumanne na ametaka zoezi la kuhesabu
kura lianze upya. Bi. Banda ambaye yumkini akapoteza cheo chake amesema
miongoni mwa udanganyifu uliothibitishwa na mawakala wa chama chake ni
pamoja na mtu mmoja kupiga kura zaidi ya mara mbili, wagombea fulani wa
urais kupata kura nyingi zaidi zisizoendana na idadi ya wapiga kura
waliojiandikisha katika baadhi ya maeneo pamoja na kudukuliwa kompyuta
za tume ya uchaguzi. Hata hivyo, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Maxon
Mbendera, amekanusha madai ya kudukuliwa tarakilishi za tume hiyo
akisema kilichofanyika ni mitambo kuvurugika. Mbendera amesema baada ya
mitambo ya elektroniki kufeli kufanya kazi, wameamua kuhesabu kura kwa
mikono na ameahidi kwamba matokeo yatatangazwa punde baada ya zoezi hilo
kukamilika.
0 comments:
Chapisha Maoni