Jumapili, Mei 25, 2014

JITIHADA ZA KUTAFUTA CHANJO YA UGONJWA WA MALARIA ZAZAA MATUNDA

Watafiti wa Marekani wamebaini miili ya watoto hao hutoa viini vya kinga ambavyo hushambulia wadudu wanaosababisha Malaria.
Kwa kumdunga mtu sindano yenye viini hivyo vyo mtu anaweza kukingwa na ugonjwa huo .

Watafiti hao ambao walichapisha matokeo yao kwenye jarida la kisayansi , wanasema majaribio ya utafiti huo katika binadamu na katika sokwe sasa yanahitaji kutathminiwa kikamilifu ili kupata matumaini halisi ya chanjo ya malaria.
Prof Jake Kurtis, mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa afya wa kimataifa katika hospitali ya kisiwa cha Rhode katika chuo kikuu cha tiba cha Brown , alisema : 
Nadhani kuna ushahidi wa kuaminika kwamba hii inaashiria upattikanaji wa chanjo
Hata hivyo wadudu wa malaria ni vigumu kuwashambulia. Kwa kweli ni maadui wakubwa .
aliongeza Kurtis. Utafiti huo ulianza kwa kundi la watoto wa shule 1000 nchini Tanzania , ambao sampuli za damu yao zilichunguzwa mara kwa mara katika miaka ya mwanzo ya maisha yao .
Asilimia 6 ya watoto ya watoto hawa waliweza kuwa na kinga asilia kwa malaria, licha ya kuishi katika eneo ambako ugonjwa huo umekithiri.

0 comments:

Chapisha Maoni