Jumanne, Mei 13, 2014

JIPYA LA TUNDU LISSU KUHUSU MUUNGANO!

Alichokiandika Tundu Lissu kuhusiana na suala la muungano kupitia ukurasa wake wa facebook  ni hiki:

Sisi wa KIZAZI cha Muungano tunataka kuujua ukweli juu ya makosa waliyoyafanya hawa WAASISI wetu wa Muungano hadi wakauawa na Kuzikwa katika HANDAKI moja kwenye Eneo linaloitwa kama nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Waasisi hao ni Abdallah Kassim Hanga aliyekuwa Waziri Mkuu, Abdulaziz Twala aliyekuwa Waziri wa Fedha na Saleh Akida aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, wengine walikuwa Viongozi waandamizi wa Serikali ya Mapinduzi ambao ni Othman Shariff, Mdungi Ussi na Jaha Ubwa. Ushahidi wa haya yote upo kwenye Kitabu cha "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru"kilichoandikwa na Harith Ghassany. Waheshimiwa naomba kuwasilisha hoja!

0 comments:

Chapisha Maoni