Ijumaa, Mei 09, 2014

CHANGAMOTO MPYA NA KUBWA ZA MBUNGE MGIMWA KALENGA

Wananchi wa Jimbo la Kalenga Mkoani Iringa waendelea kukumbwa na changamoto ya kuzipata huduma mhimu za kijamii licha ya Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mh: Godfley Mgimwa aliyeapishwa May 6,mwaka huu,kutembelea baadhi ya Kata katika jimboni humo na kuto misaada mbalimbali kutoka kwenye mfuko wa Jimbo.
Wakizungumza kwa wakati tofauti Wananchi wa Kijiji cha Mgera Kata ya Kiwere,Wilaya Iringa wamesema pamoja na kuwepo kwa shida ya zahanati,umeme,ubovu wa barabara,lakini maji ndio limekuwa tatizo kubwa zaidi Kijiji hapo ambapo ina walazimu kulipia kiasi cha pesa ili kupata maji wakati mwingine kukosekana kabisa.
Kwa upande wa Bw:Jomo Mahenge mmoja wa wananchi hao amesema tayari mbunge wao walio mchagua machi16,mwaka huu ametembelea katika kata hiyo lakini cha kushangaza hakufika kujionea adha ya maji wanayo ipata kijini hapo ambapo kwa miezi mitatu sasa mtambo wa kuvutia maji ulikua haufanyi kazi na badala yake alitembelea vijiji vingine,huku wao wakitumia muda mwingi kumsubiri.
Naye Mhasibu wa maji kijijini hapo Bi: Esta Nyaulingo amekiri kupokea kiasi cha shilingi 100 toka kwa wanachi wakati wa kupati huduma ya maji na kuongeza kuwa fedha hizo hutumika kwa ajiri ya ukarabati wa mtambo na kununua nishati ya mafuta ambapo toka Jully hadi Novemba 2013 walikusanya kiasi cha zaidi ya sh milioni 1.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw: Pasco Speso amekiri kuwepo kwa tatizo la maji,pia ameongeza kuwa mpaka kufika May 8 mwaka huu wamesha tengeneza mtambo wa kuvuta maji ambao ulioharibika miezi 3 iliyopita hivyo itasaidia kupunguza tatizo hilo na kuwataka wananchi kuendelea kuchangia kiasi cha sh 100 kwa kila ndoo 1 ya maji huku akiwaasa kuyachemsha maji hayo kabla ya kuyatumia.
Hata hivyo kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Kiwere Mh: Pasko Mwano amekili kuwepo kwa changamoto hizo,ambapo tayari wamesha kutana na mamlaka ya maji safi na majitaka Iringa(IRUWASA) ili kuona namna ya kupata huduma hiyo,na kuongeza kuwa katika kijiji hicho tayari wananchi wamekwisha andaa tofari kwa ajiri ya ujenzi wa zahanati.

0 comments:

Chapisha Maoni