Kuna taarifa kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand,
Yingluck Shinawtra, ameachiliwa huru na viongozi wapya wa jeshi, siku
mbili baada ya kuwekwa kizuizini.
Duru ndani ya baraza la kijeshi linaloongoza
nchi, zimeliambia BBC, kwamba Bibi Shinawtra, ameambiwa asijishughulishe
na siasa, na anahitaji kibali akitaka kutoka nje ya nchi.
Bi Shinawtra alikuwa mmoja kati ya wanasiasa,
wasomi na wadadisi, kama mia-moja-na-50, ambao walifungwa baada ya jeshi
kunyakua madaraka Alkhamisi.
Wengi bado wako kizuizini.
Maandamano madogo lakini ya hasira, yameendelea
kwa siku ya tatu mjini Bangkok, na kuzusha mapigano na baadhi ya watu
kukamatwa, lakini hapakuwa na mapambano makali na askari wa usalama.
0 comments:
Chapisha Maoni