Polisi nchini Uhispania, wanasema wamemkamata shabiki
aliyemtupia mchezaji soka wa Barcelona Dani Alves Ndizi siku ya
Jumapili akiwa uwanjani.
Dani ni raia wa Brazil anayesakatia soka yake katika klabu ya Barcelona.
Kitendo hicho cha ubaguzi kilitokea wakati Alves alipokuwa anajiandaa kupiga mpira wa kona uwanjani siku ya Jumapili.
Alves alichukua Ndizi hiyo na kuila, kitendo
ambacho kimemletea sifa duniani kote na hata kuanzisha kampeini dhidi ya
ubaguzi wa rangi katika mitandao ya kijamii.
Shabiki huyo aliyekamatwa anajulikana kama David Campaya na ana umri wa miaka 26 anayeunga mkono klabu ya Villarreal.
Alves amesema kuwa amekuwa akipinga vitendo vya ubaguzi kwa miaka sita
Klabu hiyo ilisema kwamba mwanamume huyo hataruhusiwa tena kuhudhuria mechi zozote msimu huu na kwamba amepigwa marufuku maisha.
Mchezaji huyo alisema alishangazwa sana na
uungwaji mkono aliopata kutoka kote duniani watu wengi wakionekana
kwenye mitandao ya kijamii wakila Ndizi kama ishara ya kumuunga mkono
Alves.
Barcelona walishinda Villareal mabao 3-2 katika
mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa El Madrigal mjini Castellon
pwani ya Hispania.
Alves aliambia BBC kuwa kilichomkumba sio jambo geni, na kwamba amekuwa akipinga vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa miaka sita.
0 comments:
Chapisha Maoni