Alhamisi, Aprili 10, 2014

VANESSA MDEE AFANYA BONGE LA COLLABO NA MNIGERIA

December mwaka jana (2013) mwimbaji wa Tanzania Vanessa Mdee aka Vee Money alienda nchini Nigeria na kupanda jukwaa moja na wasanii wakubwa wa nchi hiyo akiwa ni msanii pekee wa Tanzania, katika show kubwa ya kila mwaka iitwayo ‘Harp Rhythm Unplugged’.
Safari hiyo ilikuwa na lengo la kupanda mbegu za muziki wake katika ardhi ya kimataifa, mbali na kufanya interviews pia alifanikiwa kufanya collabo na msanii wa Naija.
Vanessa amezungumza leo na kuthibitisha juu ya habari hiyo njema kuwa amefanya collabo na msanii wa Naija, lakini habari mbaya ni kuwa hajawa tayari kumuweka wazi msanii huyo hadi muda wa kutoa wimbo huo utakapofika.
“…Single moja kubwa ambayo inatoka hivi karibuni na msanii mmoja wa Nigeria, sipendi kutangaza mambo hadi yawe yamefikia”. Alisema Vee.
Nilipomuuliza kama ni Iyanya ambaye waliwahi kuonekana karibu alipokuja Tanzania kwenye Fiesta mwaka jana, jibu lake lilikuwa (kicheko) kisha “hapana”.
Vee Money ambaye single yake ya ‘Come Over’ ilifanikiwa kuingia katika chart ya radio ya Nigeria ‘The Beat 97.9fm’, amesema collabo hiyo ilifanyika Nigeria na baadaye alikuja kuimalizia hapa Tanzania. “tulianza kidogo nilipokuwa huko and then nimemalizia hapa”.

0 comments:

Chapisha Maoni