Rais wa Uganda Yoweri Museveni,amemkabidhi mfalme wa Buganda mali ambayo ufalme huo ulipokonywa mnamo miaka ya sitini.
Mali hiyo ambayo ni pamoja na ardhi, majumba na
hati za kumiliki ardhi ilikabidhiwa kwa mflame wa Buganda katika sherehe
iliyofanywa mjini Kampala.
Buganda ndio ufamle mkubwa wa
kitamaduni uliosalia nchini humo. Ulifutiliwa mbali na aliyekuwa Rais
Milton Obote mwaka 1966 lakini ukarejeshwa tena na Rais Museveni mapema
miaka ya tisini.
Rais Museveni alikabidhi nyaraka za umiliki wa
mali hiyo kwa naibu mkuu wa Katikiro au waziri mkuu wa ufalme huo
Emmanuel Sendaula katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Rais mjini
Entebbe.
Kadhalika Rais Museveni alisifu ushirikiano uliopo kati ya utawala wa Kabaka na serikali.
Museveni aliongeza kuwa uhusiano kati ya pande
hizo mbili utasalia kuwa mzuri na kwamba vizingiti vilivyokuwepo
vimeondolewa na kuwa Rais hataki mzozo wa kijamii.
Alisema Kabaka Ronald Mutebi wa pili, anaweza kuzuru Kayunga bila wasiwasi wowote.
0 comments:
Chapisha Maoni