Alhamisi, Aprili 17, 2014

SOMA HAPA HABARI YA MSICHANA WA MIAKA 15 ALIYEOKOLEWA BAADA YA KUFUNGIWA MIAKA TISA KATIKA CHUMBA AKIISHI NA MBWA PAMOJA NA TUMBILI

Polisi nchini Argentina wamemwokoa msichana mwenye umri wa miaka kumi na mitano ambaye alifungiwa katika chumba cha kuegesha magari na kunyimwa chakula pamoja na kupigwa na wazazi waliokuwa wamemuasili, kwa kipindi cha miaka tisa.
Msichana huyo alikuwa na uzani wa kilo ishirini pekee.

Viumbe wa pekee walioishi naye ni mbwa pamoja na Tumbili. Msichana huyo amesema alipigwa kila mara iwapo angejaribu kula mabaki ya chakula kilichotupwa kwa wanyama hao.
Amesema alifanikiwa kuondoka katika eneo hilo la kuegesha magari mara mbili tu katika kipindi cha miaka tisa.
Walezi wake wamekamatwa na kufunguliwa mashItaka ya kumdhulumu na kumweka kama mtumwa msichana huyo.
Msichana huyo ambaye amelazwa hospitlaini, alipatikana na dadake wa kuzaliwa naye mjini Buenos Aires.
Kwa mujibu wa maafisa wakuu, wazazi hao walimuasili mwaka 2001 baada ya mahakama kuamua kuwa wazazi wake wa kumzaa hawakuwa na uwezo wa kifedha kuweza kumlea.
Walikuwa wanasubiri stakabadhi za kukamilisha mpango wa kumuasili mtoto huyo.

0 comments:

Chapisha Maoni