Jumanne, Aprili 29, 2014

PETER OKOYE WA P-SQUARE ATUMIA ZAIDI YA MILIONI 300 KUNUNUA GARI

Kama unakumbuka vizuri nilikuletea habari mbili tofauti kuhusu mzozo katika familia ya vipaji Afrika, familia iliyowatoa mapacha wawili wa P-Square nchini Nigeria na zikasomwa sana kutokana na watu hao kuwa na mashabiki wengi sana duniani...sasa leo kipo kingine kikubwa sana, unafafikiria nini unapoambiwa mtu kanunua gari kwa zaidi ya sh.300 milioni pesa ya kitanzania?
Baada ya kumaliza matatizo yao kwenye familia na ndugu zake ambayo bado hayajajulikana kama yalikuwa ni kweli au ni stunt za biashara yao kwenye muziki, Peter amewaonyesha fans wake gari lake jipya lililomtoa zaidi ya milioni 300 kwenye pesa za kitanzania. Peter na ndugu zake wawili ilisemakana hawakuwa kwenye maelewano kwa kipindi kifupi lakini baadae wote watatu wali-tweet maneno ambayo yaliashiria wamemaliza tofauti zao.

0 comments:

Chapisha Maoni