Jumatatu, Aprili 14, 2014

MWIGULU NCHEMBA ATOA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WAKE WA KAZI HUKO IRAMBA


Kazi ya Kukagua Miradi ya Maendeleo,Kusikiliza Kero za Wananchi,Kuwapa mrejesho wa Ahadi nilizotoa,Imeendelea hii leo Kata ya Ntwike -Jimboni-Iramba.
Nimefanya Mikutano Minne(Mingela,Nsusu,Ntwike na Nkongilangi) kata yote ya Ntwike,
Niliwaahidi Maji Kijiji cha Mingela,Nimewapelekea na sasa Wanatumia Maji.
Niliwaahidi Umeme,Mradi Upokwenye hatua ya Utekelezaji,Vijiji Vya Jirani-Mgongo Umeshafika na Wanatumia.
Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Unaendelea Vizuri,Wananchi Wanachohitaji ni Maendeleo kwa Vitendo,Maendeleo ni Mipango.
Niliwaahidi Barabara(Uboreshaji Umeshaanza na sasa naipeleka hadi Wilaya ya Meatu.
Niliwaahidi Kuboresha Huduma ya Afya,Nimefikisha Umeme na Maji Kituo Kikubwa cha Afya cha Mgongo,Nimewapelekea Gari(Ambulance) ambayo itatumika Bure,Wananchi hawatatozwa,Kukodishwa wala Kuchangishwa Mafuta.

0 comments:

Chapisha Maoni