Jumatatu, Aprili 28, 2014

MSIGWA: VIONGOZI WA WILAYA KAENDI NA WAFANYA BIASHARA MJUE KERO ZAO

Viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa wameshauriwa kukaa na wafanyabiashara ili kujua kero na changamoto wanazokumbana nazo ili kuzipatia ufumbuzi.
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa amesema hayo kwenye kikao na wafanyabiashara wa manispaa ya Iringa ili kujua changamoto wanazokabiliana ili wafanye biashara zao kwa utulivu.
Mhe. Msigwa ameongeza kuwa pamoja na madiwani kuwa ni watungaji wa sheria ndogondogo zinapaswa kusaidia kuondoa kero zao ama atazipeleka bungeni ili kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi hususani utumiaji wa mashine za kierectriniki.
Mbunge amewashauri wafanyabiashara wa soko kuu la Mkoani Iringa kuongezewa mda wa kufanya biashara ili waifanye mpaka saa mbili za usiku kwa kuwekewa taa ndani ya soko hilo ili wafanye biashara nyakati za usiku.
Aidha Mhe. Msigwa amewakumbusha wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati ili kuondokana na changamoto ambazo zimekuwa hazifanyiwi kazi kutokana na halmashauri kutokuwa na fedha.
Hata hivyo kwa upande wa katibu wa Umoja wa wafanyabiashara wa Manispaa ya Iringa Bw. Jackon Kalole wameiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa mashine za Kieretroniki kwakuwa zinawadidimiza kiuchumi.

0 comments:

Chapisha Maoni