Muimbaji na mchezaji mahiri Msami Jiovann aka Msami ambapo ameshatoa
nyimbo nyingi ikiwemo ya ‘Unalingalinga’, ‘Nalia Na Moyo’ na kwa sasa
anatamba na audio pamoja na video ya wimbo wake wa ‘Sound Track’.
Baada ya kufanya vizuri kwa ngoma zake hizo sasa mkali huyo anahitaji meneja wa kusimamia kazi zake.Nilikaa kimya kwa mwaka jana na hii siyo kwamba niliishiwa katika music hapana ila nilikuwa nasomea muziki zaidi ili niujue kwa umakini wa kutosha.
kwa sasa ndiyo nimeingia rasmi katika muziki na nashukuru video na audio ya ”Sound Track” inafanya vizuri kwenye radio na TV Stations, kwa sasa najisimami kazi zangu mwenyewe hivyo nawakaribisha meneja ambae atakubali kufanya kazi na mimi, and all in all kwa fans wangu waendelee kuni-suport muziki wangu.
0 comments:
Chapisha Maoni