Jumatatu, Aprili 14, 2014

MISS KILIMANJARO KUFANYIKA JUNE 6

Mashindano ya Miss Kilimanjaro yanayofanyika kila mwaka katika mkoa wa Kilimanjaro,kwa mwaka huu yanatarajia kufanyika tarehe 6 June mwaka huu katika Viwanja vya Laliga Carnival.
Mratibu wa mashindano hayo Jacqueline Chuwa aliyewahi kuwa Miss Bagamoyo then Miss Kilimanjaro 2009 alisema ;
“Mashindano ya Miss Kilimanjaro ya mwaka huu yatakuwa tofauti na miaka ya nyuma kutokana na maandalizi yake, washiriki wa kinyang’anyiro hicho wamejiandaa vilivyo katika ushindani huo,na tunatarajia kuwa na idadi ya washindani 18 watakao gombania taji hilo la Miss Kilimnjaro 2014.“
aliendelea kusema;
“Mshindi wa kwanza atakayepatikana atazawadiwa shilling millioni 3,na wa pili atazawadiwa millioni 2,na watatu atzawadiwa million 1,katika mashindano hayo yatapambwa na Burudani toka kwa wasanii Dr Jose Chamelion,Dully Sykes,Sam Wa Ukweli na wenginewe kibao.”
Miss Kilimanjaro 2014 imedhaminiwa na TBL,BAABKUBWA MAGAZINE,MR PRICE,SALSALNERO HOTEL. Kiingilio kwa VIP ni Tsh 40,000 na kawaida ni Tsh 20,000, show itafanyika katika Viwanja vya Laliga Carnival, na milango itafunguliwa kuanzia saa mbili till late.

0 comments:

Chapisha Maoni