Jumanne, Aprili 29, 2014

MAKUBWA YOTE YALIYOTOKEA DUNIANI TAREHE KAMA YA LEO NA KUWEKA HISTORIA

Leo ni Jumanne tarehe 29, Miaka 69 iliyopita katika siku kama ya leo majeshi ya Muungano yalipata pigo kubwa mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia. Vikosi vya nchi Waitifaki wa Ulaya vilifanya mashambulizi ya pande zote dhidi ya Italia baada ya kusambaratishwa safu ya ulinzi ya Ujerumani. Italia ilikuwa muitifaki wa Ujerumani chini ya uongozi wa Musolini. Baada ya ushindi huo askari karibu milioni moja wa Ujerumani waliokuwa nchini Italia walijisalimisha kwa majeshi ya Waitifaki.

Siku kama ya leo miaka 86 iliyopita sawa na tarehe 29 mwezi Aprili mwaka 1928, nchini Uturuki herufi za Kilatini zilitambuliwa rasmi na kuchukua nafasi ya zile za Kiarabu. Hatua hiyo ilichukuliwa katika njama za kuipiga vita dini ya Uislamu na badala yake kuingizwa tamaduni za Kimagharibi katika jamii ya wananchi wa Uturuki. Mchakato huo ulianzishwa na Mustafa Kamal maarufu kwa jina la Ataturk kuanzia mwaka 1923. Mfumo wa Jamhuri ulishika hatamu za uongozi huko Uturuki chini ya Ataturk kuanzia mwezi Oktoba mwaka 1923 baada ya kuanguka kwa utawala wa Othmania uliodumu kwa miaka 623 nchini humo.

Na siku kama ya leo miaka 1399 iliyopita sawa na tarehe 29 Jamadithani mwaka 36 Hijria kwa mujibu wa baadhi ya wanahistoria akiwemo Masoudi, vilianza vita vya Jamal kati ya jeshi la Imam Ali bin Abi Twalib AS na kundi la waasi lililokuwa likiongozwa na Talha na Zubeir. Kundi hilo lilianzisha uasi huo baada ya kushindwa kustahamili msimamo uliyoonyeshwa na Imam Ali AS wa kutekelezwa uadilifu katika jamii. Awali kundi hilo lilikuwa limekula kiapo cha utiifu kwa Imam Ali AS, lakini likaamua kuasi baada ya kushindwa kufikia malengo yake batili, na kuanzisha vita kwa kisingizo cha kulipiza kisasi cha damu ya Othman bin Affan.

0 comments:

Chapisha Maoni