Jumanne, Aprili 15, 2014

MAJANGA! MUHIDIN GURUMO HAKUTAKA KUZIKWA

Muhidin Mohamed Mwalimu Gurumo ‘Maalim Gurumo’ amezikwa jana kwenye makaburi ya kijijini kwake, Masaki, Kisarawe mkoani Pwani, lakini wosia aliouacha kuhusu mazishi yake umezua utata.
Kwa mujibu wa chanzo, wakati wa uhai wake Maalim Gurumo ambaye alikuwa mwanamuziki wa bendi mbalimbali nchini, ikiwemo Ottu na baadaye Msondo Music Band, alisema atakapotangulia mbele ya haki asizikwe siku inayofuata.
Kwa mujibu wa chanzo, Gurumo alimpa wosia huo mjomba’ake aitwaye Selemani Mikole ambaye ndiye aliyemlea alipofika jijini Dar es Salaam baada ya kufiwa na baba yake mzazi, mzee Mohamed Mwalimu Gurumo.
“Gurumo alikataa kuzikwa siku inayofuata. Mjomba wake ndiye aliyetoa siri hiyo mara baada ya Gurumo kufariki dunia.
“Yaani alitaka hivi, mfano amefariki dunia leo (jana Jumanne) basi mazishi yake yawe baada ya siku mbili, yaani keshokutwa (Alhamisi).
“Mjomba’ake alimuuliza sababu ya uamuzi huo, akasema yeye ni mtu mwenye mashabiki wengi, angeomba pawe na muda ili wengi waweze kuhudhuria mazishi yake,” kilisema chanzo hicho.

Jumatatu iliyopita kwenye msiba wa nguli huyo nyumbani kwake, Mabibo-Makuburi jijini Dar es Salaam baadhi ya waombolezaji wenye imani ya Kiislam walisikika wakipingana na wosia huo wa marehemu. Baadhi walisema si sawa Muislam kuzikwa baada ya saa ishirini na nne huku wengine wakisema wosia wa marehemu ndiyo maelekezo makuu ya mazishi.
 “Hapa hatuzungumzii sheria za dini, tunazungumzia kutii wosia wa marehemu. Siku zote wosia wa marehemu unazingatiwa kwanza,” alisikika akisema mwombolezaji mmoja baada ya kuambiwa mazishi ya marehemu huyo ni Jumanne na si Jumatatu kama alivyoamini.

0 comments:

Chapisha Maoni