Milipuko miwili imetokea katika kituo cha mabasi
katika vitongoji vya mji mkuu wa Nigeria, Abuja, na kuna taarifa ya watu
wengi kujeruhiwa kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo.
Mwandishi wa BBC, nchini Nigeria, Haruna Tangaza
anasema milipuko hiyo ilitokea wakati abiria wakiwa katika harakati za
kupanda mabasi na teksi wakienda maofisini katikati ya mji wa Abuja.
Shirika la habari la Uingereza,
Reuters, limewakariri watu walioshuhudia tukio hilo wakisema mabasi
mawili yaliyokuwa yamejaa abiria yalilipuliwa.
Mmoja wa mashuhuda wa shambulio hilo, Badamsi Nyanya ameiambia BBC kuwa ameona miili 40 ikiondolewa.
"Asubuhi hii kulikuwa na mlipuko katika eneo la
maegesho ya magari ya Nyanya Motor Park," anasema Manzo Ezekiel wa
Wakala wa Usimamizi wa Taifa wa Majanga.
Vikosi vya uokoaji tayari vipo katika eneo la tukio.
Shuhuda mwingine Bi Mimi Daniels, ambaye
anafanya kazi mjini Abuja, anasema: "nilikuwa nasubiri basi niliposikia
mlipuko mkubwa halafu nikaona moshi," ameiambia Reuters.
"Watu walikuwa wakikimbia ovyo kutokana na taharuki."
0 comments:
Chapisha Maoni