Shirika la Fedha Duniani IMF limeidhinisha msaada wa
dola bilioni kumi na saba kuunusuru uchumi wa Ukraine wakati taifa hilo
likijitahidi kurejesha utulivu wa kisiasa na kiuchumi.
Msaada huo ulioahidiwa mnamo mwezi Marchi
utategemea mabadiliko makubwa ya kiuchumi, ikiwemo kupanda kwa kiwango
cha kodi na bei ya nishati mbali na kupigwa tanji kwa mishahara ya
chini.
Zaidi ya dola billioni tatu zitakabidhiwa mara
moja serikali ya Ukraine ambayo inakabiliwa na mzozo wa kiuchumi pamoja
na kisiasa.
Awali mkutano wa kimataifa uliofanyika mjini
London ulikamilika na ahadi ya kuisadia Ukraine kuisaka mali ya
mamilioni ya madola inayodaiwa kuibwa na aliyekuwa kiongozi wa taifa
hilo Victor Yanukovych pamoja na wandani wake.
0 comments:
Chapisha Maoni