Mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Grace Sarakikya amedai kuwa
tarehe 14 mwezi huu wa Nne alitekwa na Msanii Bongo flava Ney wa Mitego
maeneo ya Kimara, Grace anadai kuwa kabla ya kutekwa alikua anawasiliana
na rafiki wa Ney anayeitwa Bonge lakini awali hakujua kama anafahamiana
na Ney.
Sababu ya kuwasiliana na Bonge amesema kuwa Bonge ni camera man na walifahamiana kupitia mtandao wa Instagram na Bonge
aliahidi kumpa dili la kuigiza kwenye filamu, wakakubaliana acheze
Scene 20 kwa malipo ya elfu 50 kila Scene, Sasa siku hiyo ya tukio
wakapanga kukutana Kimara, Mwanadada Grace akaibuka mpaka kimara akiwa
amekodi pikipiki a.k.a Bodaboda lakini kabla ya kufika huko dereva
bodaboda alishamtahadharisha kuwa maeneo wanayoenda sio salama.
Kufika kule akakutana na Bwana Bonge lakini ghafla Ney wa Mitego
akajitokeza na kumuamuru Bodaboda asepe lakini jamaa alichomoa na
kuwaambia lazima aondoke na mteja wake, basi mwanadada akawekwa chini ya
Ulinzi na kuamuriwa amuombe msamaha Girlfriend wa Ney anayeitwa Siwema
kwa madai kuwa Grace kwa kushirikiana na watu wengine wamekua
wakimtukana sana Ney pamoja na Siwema kwenye Instagram.
0 comments:
Chapisha Maoni