Jumamosi, Aprili 26, 2014

HII NDIO POST KALI ZAIDI LEO KUTOKA FACEBOOK

KUNA WIZI UMETOKEA BENKI
••••••••••••••• •••••••
Jambazi akasema "wote laleni chini pesa ni za serikali na maisha ni ya kwenu", wote wakalala chini (HII INAITWA DHANA ...YA USHAWISHI - kubadilisha njia ya kawaida ya kufikiria)
••••••••••••••• •••••••
Kuna dada kwa woga akawa amelala chini kimitego, Jambazi akamwambia, "dada hebu kuwa na adabu chukua kanga jifunike hili ni tukio la ujambazi na sio la ubakaji.” (HUU UNAITWA WELEDI -zingatia ulichofundishwa kufanya)
••••••••••••••• •••••••• Walipotoka kwenye wizi jambazi mdogo ambaye ana shahada ya uzamili ya biashara akamwambia mwenzake, "tuzihesabu hizi fedha.” Yule mkubwa akamcheka
kwa dharau na kumjibu, "wewe
mjinga sana hizo hazina haja ya kuhesabu saa mbili wata tutangazia kwenye taarifa ya habari tumeiba kiasi gani. (HUU INAITWA UJUZI - Siku hizi ujuzi ndio bora kuliko vyeti)
••••••••••••••••••••••• Baada ya majambazi kuondoka meneja akamwambia mhasibu wa bank, " ujumlishie na zile milioni 80 tulizo iba sisi.” (HUKU KUNAITWA KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI - kushabihiana na mazingira magumu kwa faida binafsi.)
••••••••••••••• ••••••••
Mhasibu akafurahi na kusema, "dah wizi ukitokea kila mwezi itakuwa burudani sana.” (HUKU KUNAITWA KUWA NA MAWAZO CHANYA - Furaha ndio kitu cha muhimu zaidi)
•••••••••••••••••••••• Meneja kafurahi sana kwa kuwa sasa matatizo yake yametatuliwa
na wizi uliojitokeza. (HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU-shiki lia nafasi pale inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi gani.

••••••••••••••• •••••••• Haya usiku wake taarifa ya habari
ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa million 100 umetokea leo benki. Majambazi kuskia hivyo wakaanza kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta na milioni 20 tu.
Yule jambazi mkubwa akashtuka na kusema, "dah! yaani meneja kaiba mara nne zaidi yetu bila kuchezesha msuli? Bora umeneja kuliko ujambazi.” (HII INAITWA
ELIMU NDIYO KILA KITU - ishike sana elimu ina nguvu kuliko chochote.)

0 comments:

Chapisha Maoni