Ijumaa, Machi 14, 2014

WENGER: MESUT OZIL OUT!!!

Meneja wa Arsenal,Arsene Wenger amethibitisha kuwa Mesut Ozil atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu mpaka sita kutokana na kupata majeraha ya misuli kwenye mchezo waliotoka sare ya goli 1-1 dhidi ya  Bayern Munich.
Kiungo huyo wa kijerumani alitolewa katika kipindi cha kwanza Jumanne usiku kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya uliopigwa Allianz Arena na tayari atakosa mchezo wa wapinzani wa Jiji dhidi ya Tottenham siku ya Jumapili.
Mfaransa huyo alisisitiza kuwa,”Tumempoteza Ozil,ambaye amekuwa majeruhi kwa kukosa mchezo wa Jumapili,Sifahamu atakuwa nje kwa kipindi gani lakini inaweza kuchukua wiki kuanzia tatu.”
Na kuongeza,”Kama wastani ni wiki tatu basi inaweza kufikia wiki sita.Sina uzoefu mkubwa wa kufahamu hilo zaidi ila ni tatizo la misuli ya paja hivyo labda tuseme wiki nne.”

Kukosekana kwa Ozil kumekuja mara baada ya taarifa za Aaron Ramsey kutokuwa fiti bado licha ya kuanza mazoezi pamoja na Jack Wilshere ambaye naye bado anauguza majeraha ya kifundo cha mguu aliyopata kwenye timu yake ya Taifa ya Uingereza.
Lakini kiungo mpya raia wa Sweden,Kim Kallstrom huenda akawepo White Hate lane kucheza mchezo wake wa kwanza mara baada ya kusajiliwa kwa mkopo huku akiwa majeruhi akitokea Spartak Moscow naye Nacho Monreal anataraji kurejea.
Wenger aliongeza kuwa,”Ukweli ni pigo lakini najiamini tunaubora wa kuweza kupambana bila Ozil.Tunawachezaji wengi hodari ambao wanaweza kuchukua nafasi na kuonyesha kiwango kizuri.

0 comments:

Chapisha Maoni