Jumatatu, Machi 17, 2014

NJAMA ZA UGAIDI ZAFICHUKA, POLISI WAKAMATA MABOMU NDANI YA GARI

Polisi mjini Mombasa pwani ya Kenya wamewakamata watu wawili waliokuwa na mabomu waliyoyatengeneza ndani ya gari lao
Kwa mujibu wa polisi washukiwa hao mmoja raia wa Kenya na mwingine msomali, walikuwa wanajiandaa kufanya mashambulizi katika eneo lisilojulikana.
Inaarifiwa polisi waliwakamata baada ya kupata taarifa kuhusu njama yao.
Vyombo vya habari vinasema kuwa usalama umedhibitiwa mjini humo kufuatia tukio hilo.

0 comments:

Chapisha Maoni