Jumatatu, Machi 10, 2014

MFUMO WA AFYA SYRIA WASAMBARATIKA

Shirika la Misaada la “Save the Children” limeonya kuwa mfumo wa kiafya wa Syria uko katika hali ya kusambaratika na kwamba watoto wadogo wanataabika kutokana na kukosekana huduma za afya zinazohitajika.

Shirika hilo la hisani limesema katika ripoti yake ya jana kuwa, karibu asilimia 60 ya hospitali huko Syria zimebomolewa au kuharibiwa tangu kuzuka machafuko nchini humo miaka mitatu iliyopita na kwamba karibu nusu ya madaktari wameikimbia nchi hiyo.
Shirika la hisani la “Save the Children” limekutaja kusambaratika kwa mfumo wa afya wa Syria kuwa ni jambo la kutisha na kuongeza kuwa idadi ndogo ya wafanyakazi wa sekta hiyo wanahangaika kuwahudumia raia wanaojeruhiwa kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo.

0 comments:

Chapisha Maoni