Nyota wa muziki wa kizazi kipya, Esterlina Sanga ‘Linah’
ametoa mpya baada ya kuibuka na kueleza wazi kuwa, afanyapo mapenzi hapendi
kutumia kinga.
Linah alisema hayo wakati akizungumza na Fichuo ambapo amesisitiza kuwa
anachukia sana mipira ya kike na kiume wakati wa tendo kwa vile
zinamkata stimu.
“Sema naogopa ukimwi na magonjwa mengine ndiyo maana nalazimika
kutumia kwa ajili ya afya yangu lakini kiukweli kabisa, sipendi kabisa
kinga,” alisema Linah.
Hivi karibuni, nilikupatia story ya staa huyo wa muziki
kudungwa mimba na mdosi kabla ya siku chache baadaye kugundulika kuwa,
kiumbe chake kilichoropoka.




0 comments:
Chapisha Maoni