Jumapili, Machi 16, 2014

HIVI NDIVYO SMS ZAKO ZINAWEZA KUSOMWA KATIKA WHATSAPP BILA RUHUSA YAKO

Kwa hivi sasa inasemekana ni rahisi sana kwa mtu kuweza kusoma message za mtu mwingine za whatsapp kupitia baadhi ya application mbali mbali za kudownload za android.
Whatsapp hivi sasa imekuja na mechanism ya kuweza kufanya backup ya message zako zote na kuzihifadhi online wakati unapotaka ku-uninstall au ku-install,kwa kukupa code ambayo inampa kila mtu duniani kwa wakati tofauti,badala ya kumpa kila mtumiaji code ya siri tofauti nay a mtu yeyote duniani.
Kutokana na research iliyofanywa na mashable.com,hii inamaanisha kuwa hiyo backup yako inaenda kuhifadhiwa kwenye database ambayo haina security yakutosha,risk inayofanya backup yako iweze kusomwa na mtu yeyote mwingine mwenye app nyingine mbali na whatsapp,sababu hii inakuja kwa kile kinachosemekana kuwa kuna watengenezaji wa apps wameweza kupata access ya backup hizo kupitia application zao.
Na kwa wale wanao-penda kuhifadhi backup ya whatsap kwenye memory card zao za simu,hii ndio njia rahisi kuliko yote kwa mtu yeyote atakaye pata memorycard yako,kwa kutumia application nyingine ya android, anaweza kusoma message zako za whatsapp vizuri tu bila shida yeyote ile.

0 comments:

Chapisha Maoni