Katika ufuo wa bahari ya Ziwa Viktoria kuna biashara
inayovuma-dau za uvuvi zilizotengenezwa kwa mbao zimejaa si haba,
asubuhi zimejazwa Samaki wa Tilapia.
Nyakati za asubuhi na mchana, wavuvi hukusanyika
na kupiga foleni kununua Samaki; wengi wao wakiwemo wanawake ambao
wanatumainia kupata faida; japo kidogo, katika soko lililo karibu.
Ila, katika sehemu hii ya Kenya, biashara hii haifanywi kwa ubadilishanaji wa pesa kwa Samaki.
Malipo ni ubadilishanaji wa ngono kwa Samaki: wanawake wanauza miili yao kwa matumaini kuwa wataeleka nyumbani na Samaki wengi.
Biashara hii inajulikana kama “ubadilishanaji wa ngono kwa samaki” ama, kwa lugha ya kiluo, inajulikana kama “jaboya”.
Lucy Odhiambo, 35, anatayarisha ununuzi wake wa
mwisho, ambao ataupeleka sokoni; anawapasua samaki na kuwatoa uchafu wa
tumboni. Ni mjane, na mama wa watoto tano, anasema kuwa wanawake hapa
wanalazimika kufanya wasiyotarajiwa kufanya na jamii.
"Inanilazimu niuuze mwili wangu kwa wavuvi ili nipate samaki kwa sababu sina uwezo wa kujikimu".
"Kawaida, mimi hulala na wavuvi wawili au watatu
kwa juma. Naweza pata magonjwa, ila sina budi kufanya hivyo. Nina
watoto ambao nafaa kuwalipia karo. Jaboya ni tendo baya mno. "
Ugonjwa anaouongelea hapa ni ukimwi ambao
umeenea sana katika eneo hili. Ripoti za afya zinadhihirisha kuwa
ugonjwa wa Ukinmwi umekithiri katika eneo hili ukiipiku kwa 15% maradufu
ile idadi ya wastani ya nchi. Hii inatokana na biashara hii ya
“ubadilishanaji wa ngono kwa samaki.



0 comments:
Chapisha Maoni