Jumatatu, Februari 10, 2014

SASA TANZANIA IMEJIBU KASHFA ZA RWANDA

Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda umeeleza kusikitishwa na taarifa za blog ya Rwanda “News of Rwanda”  ambayo inaunga mkono serikali ya nchi hiyo  iliyotolewa mwishoni mwa juma zikimtuhumu rais wa Tanzania Jakaya  Kikwete kwa kuunga mkono na kufanya mikutano na wanachama wa makundi ya waasi yanayopingana na serikali ya Rwanda. 
Akizungumza na Sauti ya Amerika mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania Salva Rweyemamu amesema  wao wameshangazwa kwa sababu mwaka jana kulikuwa na matatizo  na marais wa nchi hizo wameshazungumza  vizuri wakakubaliana  na kuonyesha kwamba sasa mambo yameisha na kwamba wanaendeleza urafiki wao, udugu wao na ujirani mwema wa miaka mingi kati yao na kuongeza kwamba hilo ni jambo la kusikitisha sana kwa upande wa Tanzania.
Ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini humo visaidie kujenga uhusiano mwema na visiwe mwanzo wa choko choko ya kugombanisha watu akiuliza kuwa “Tanzania wakigombana na Rwanda magazeti yatauzwa?” au mkiwa kwenye hali ya vurugu kama ilivyo nchi zingine ambapo watu wanapigana kila siku kuna watu wananunua magazeti pale?

0 comments:

Chapisha Maoni