Mbunge mmoja wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambaye
alikuwa katika mstari wa mbele kupinga mauaji ya Waislamu nchini humo,
ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.
Jean-Emmanuel Ndjaroua aliuawa na watu waliokuwa
wamejihami kwa bunduki waliokuwa wakitumia pikipiki, siku moja tu baada
ya kutoa hotuba kulaani mauaji yanayoendelea nchini humo.
Msemaji
wa shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights Watch, Peter
Bouckaert ameonya kuwa hali nchini humo inaendelea kuwa mbaya kila uchao
na raia wote wa nchi hiyo ambao ni Waislamu huenda wakalazimika
kutoroka katika kipindi cha wiki chache zijazo.
Maafisa wa kutoa misaada ya kibinadam wamesema
kuwa watu tisa wamefariki dunia kufuatia mapigano makali na uporaji
uliotokea katika mji mkuu jamuhuri ya afrika ya kati wikendi iliyopita.
Ripoti zinasema kuwa watu wawili wanaoaminika kuwa waislamu waliuawa kinyama wakati wa machafuko hayo.
Vita vikali vilitokea siku ya Jumamosi kati ya
wanamgambo wa Kikristo na Waislamu Magharibi mwa mji mkuu wa Bangui
ambapo majengo kadhaa yaliharibiwa kwa kuteketezwa.



0 comments:
Chapisha Maoni