Kwa mujibu wa staa wa filamu ambaye aliachwa katika safari hiyo ya
kwenda kuhamasisha sanaa itambuliwe kwenye mchakato wa katiba mpya,
Mwakifwamba alimteua Batuli ili akajiachie naye Dodoma kwa sababu hakuwa
na vigezo.
“Akina Monalisa (Yvone-Cherry Ngatikwa) walistahili kwa ukongwe wao
kwenye fani, sasa Batuli aliingiaje? Akili za kuambiwa changanya na
zako,” alisema msanii huyo.
Akizungumzia skendo hiyo, Mwakifwamba alidai kuwa ameshasingiziwa
vitu vingi hivyo anajua nyuma yake kuna kundi linalomchafua kila kukicha
lakini ukweli ni kwamba hakumteua Batuli kwa lengo hilo.
“Sasa kama nimemteua kwa sababu hiyo, je, akina Monalisa nao
niliwateua kwa kigezo hicho?” alihoji Mwakifwamba huku akikiri kuwa
ameshaisikia sana skendo hiyo.
Kwa upande wake Batuli alifunguka: “Si kweli bwana, wameshatuzushia
mambo kibao. Mara kuna fedha tumekula, mara sijui nini…sasa naona
wamekuja na hili la mapenzi. Wabongo tuache majungu.
Katika safari ya Dodoma, mbali na Monalisa, wawili hao waliambatana
na wasanii wengine wa tasnia mbalimbali wakiwemo Dude, John Kitime,
P-Funk Majani na Abdul Salvador ambapo ndani ya bunge hilo
linalotarajiwa kutikisa, wanawakilishwa na Paul Mtendah.




0 comments:
Chapisha Maoni