Kim amesema katika mechi alizofuatilia, Mbeya City ndiyo imekuwa kwenye kiwango zaidi huku timu nyingine zikitetereka katikati mwa msimu.Akizungumza na wanahabari, Kim alisema timu hiyo ni mfano wa kuigwa kwa timu zenye ndoto ya kupata mafanikio na kuuza wachezaji kama zilivyo Simba na Yanga.
“Mbeya ni mfano wa kuigwa, kwa maoni yangu ndiyo timu bora msimu huu. Wanacheza soka zuri na la kuvutia wala hawajatetereka licha ya kuwa ni timu changa.
“Ni mfano mzuri wa kuigwa kwa timu zinazotaka mafanikio na pia kuweza kuuza wachezaji kwa timu kubwa hapa nchini au nje ya nchi kama zilivyo Simba na Yanga,” alisema Kim.
Alipoulizwa licha ya kiwango chao, iweje hakuna mchezaji wa City katika kikosi cha Taifa Stars, Kim alisema: “Tuliita wanne kwenye Future Young Taifa Stars, lengo lilikuwa kuangalia uwezo wao, ukweli wana uwezo lakini wanakosa uzoefu, hivyo sikuweza kuwajumuisha kwenye timu iliyokwenda Kenya kwa kuwa tulikuwa tunapigana vita kuhakikisha tunarudi na chochote. “Naamini awamu ijayo, kutakuwa na wachezaji wengi wa Mbeya City kutokana na jinsi wanavyocheza.”
Stars inakabiliwa na mchezo mgumu wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Machi 5 mwaka huu, kwa kuchuana na Namibia mjini Windhoek.




0 comments:
Chapisha Maoni