Jumanne, Februari 11, 2014

KAMA ULIKUWA HUJUI HIKI NDICHO KIMEMFANYA WASTARA JUMA ANYWE SUMU

Kwa mujibu wa chanzo kingine cha habari, Wastara alitaka kukatisha uhai wake kutokana na kuchoka kunyanyapaliwa, kudhalilishwa na kutongozwa mara kwa mara na wanaume, hali ambayo imekuwa ikimfedhehesha mbele ya jamii.

Chanzo hicho kimesema kwamba kabla ya tukio hilo, Wastara alikuwa akilalamika kudhalilishwa na watu anaowadai fedha zake ambao hawataki kumlipa haki yake.
“Kuna watu wengi ambao Wastara anawadai lakini wanamsumbua kwa kumuona ni mwanamke asiye na nguvu na wengine wanatumia mwanya huo kumtongoza, mwenyewe anaamini haya yote yanatokea kwa kuwa Sajuki hayupo,” kimetoboa chanzo hicho.
Habari zaidi zinadai kwamba hivi sasa Amanda anaendelea kumwekea ulinzi wa karibu Wastara ili asiweze kuchukua uamuzi mbaya wa kukatisha maisha yake.
Baada ya kuyapata madai hayo, mwandishi wetu alimpigia simu Wastara ili kupata undani wa tukio hilo lakini kwa muda mrefu simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
Amanda alitafutwa ili kuweza kupata ukweli  wa madai hayo na kumuuliza kama bado yupo kwa Wastara.

0 comments:

Chapisha Maoni