Wanasayansi wanaamini kuwa unywaji mwingi wa pombe
unaweza kuleta hisia zisizo za kawaida mwilini ambazo zinaweza kuiweka
ngozi katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya ngozi.
Kemikali ya Ethanol inapogeuzwa kuwa
“Acetaldehyde” baada ya ulaji wa chakula,kemikali hii yaweza kuiwezesha
ngozi kupenyeza miale hata ya jua(UV light)
Watafiti waliofanya ugunduzi huo,
nchini Uingereza wanakubali kwamba kuna mambo mengine yanayochangia mtu
kupata Saratani ya Ngozi.
''Utafiti umeonyesha kuwa wagonjwa wanaougua
Melanoma huathirika kwa ajili ya kuota jua kwa muda mrefu,hili linaweza
kupunguzwa iwapo mtu atajikinga kutokana na jua kali,'' asema Sarah
Williams wa Utafiti wa Kansa,Uingereza.
Kulingana na utafiti wao uliochunguza mada 16
tofauti na kushirikisha maelfu ya watu,unywaji wa chupa moja ya pombe
moja au zaidi kila siku huongeza uwezekano wa kupata Saratani ya ngozi
kwa asilimia ishirini.
Uwezekano wa kupata Saratani uliongezeka sawasawa na unywaji wa pombe,kwa mfano wale waliokunywa gramu 50 ya pombe walikuwa katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya ngozi inayoua watu wengi zaidi duniani ,inayofahamika kama Melanoma.
Daktari Eva Negri,mmoja wa waandishi wa utafiti
huu kutoka chuo kikuu cha Milan anasema kuwa unywaji wa pombe unaweza
kuathiri uwezo wa mwili kujikinga hasa palipo na mnunurisho Wa miale ya
jua.
Huu unaweza kuathiri seli kwa kiwango kikubwa na hivyo basi kusababisha Saratani ya ngozi.
Utafiti huu ulinuia kujua ni kwa kiwango gani
pombe inachangia kuongeza uwezekano wa kuambukizwa Melanoma,na hivyo
basi kuwepo kwa maarifa hii inaweza kuhamasisha watu kujikinga na miale
ya jua.
Melanoma sanasana hujitokeza kwa mara ya kwa kwanza ngozini kupitia baka jeusi.
Profesa Chris Bunker,rais wa shirika la
wataalamu wa ngozi nchini Uingereza alisema kwamba Saratani ya ngozi
ndiyo kansa inayoripotiwa zaidi nchini Uingereza na inayowaua watu wengi
zaidi nchini humo.Aliongeza kuwa utafiti wowote kwa swala hili
unakaribishwa.
Wananchi wa Uingereza hufahamika sana kama
wanywaji wa pombe na wenye kupenda kuota jua,hivyo basi utafiti huu
utawaruhusu watu kufanya maamuzi bora kuhusu afya zao.
Dalili ya kwanza ya Melanoma ni kuwepo kwa baka jeusi ngozini au kubadilika kwa baka lililokuwa tayari kwenye mwili.
Hili laweza kufanyika katika sehemu yoyote mwilini hata hivyo miguu,mikono na uso huathirika pakubwa.
Kwa mara nyingi Melanoma huwa na umbo tofautitofauti na rangi zaidi ya moja.
Yaweza kuwa kubwa na mara kwa mara huwasha na kuvuja damu.
''Tunawahimiza watu kujitunza wanapokuwa chini
ya miale ya jua .Kwa kuwa watu wengi hupenda kunywa mara kwa mara
wanapobarizi,lengo letu ni kuwahamasisha kutahadhari na kukinga ngozi
zao kila wakati.''
Mara nyingi baada ya kuota jua wakati wa likizo,wengi hubambuka ngozi.
Mtaalamu Sarah Williams wa shirika la utafiti wa
SarataniKansa anasema kuwa uchunguzi huu hauelezi kikamilifu
kinachosababisha Melanoma.
Hii ni kwa kuwa watafiti wenyewe wanaeleza kuwa
,matokeo hayo ni kwa ajili ya miale ya jua wala si pombe.Utafiti nao
umeonyesha kuwa Melanoma inatokana na kuota jua kwa muda na kubambuka
ngozi:unaweza kujikinga kwa kujikinga na jua.
Kulingana na uchunguzi wake,jua nchini Uingereza
halina nguvu zaidi kusababisha Sarataniy a ngozi,hata hivyo usisahau
kukinga ngozi yako unapokwenda kupata jua wakati wa majira ya baridi.
Na kugusia swala la pombe na Saratani ya
ngozi,ni muhimu kupunguza kiwango cha pombe unachokunywa.Pombe imetajwa
kusababisha aina saba za kansa hivyo basi,kupunguza unywaji yaweza
kupunguza uwezekano wa kuambukizwa Saratani ya ngozi.
0 comments:
Chapisha Maoni