MREMBO mmoja mkazi wa Mabibo Makutano jijini Dar es Salaam (jina lake
halikupatikana) mwishoni mwa wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya
kuvamiwa na kudundwa baada ya kudaiwa kukwapua simu ya mwanaume na
kuificha sehemu zake za siri.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,
awali mrembo huyo alikuwa akila bata na mwanaume aitwaye Hashim kwenye
Baa ya Jassun Inn iliyopo maeneo ya Mabibo huku mwanaume huyo akiwa
ametandaza simu zake za kisasa juu ya meza.
Imedaiwa kuwa wakati wakiendelea kuponda raha, Hashim alikwenda
msalani kwa lengo la kujisaidia na kuacha simu zake mezani, aliporudi
hakumkuta mrembo aliyekuwa akiponda naye raha na simu yake moja
haikuwepo.
“Jasho lilimtoka Hashim na kuwauliza watu waliokaa
jirani alikoelekea mrembo huyo,” alisema shuhuda mmojawapo wa tukio hilo
na kubainisha kwamba msamaria mwema mmoja alimweleza Hashim mwelekeo wa
mrembo huyo.
Bila kuchelewa Hashim aliwakusanya wapambe wake na kuanza kumtafuta
mrembo huyo na wakamnasa mita kama 150 kutoka Baa ya Jassun na kumuuliza
kuhusu simu iliyokuwa mezani lakini alileta ubishi.
“Walijitahidi sana kumbembeleza ili aitoe simu kwa hiyari yake lakini
alikataa, ndipo Hashim na wapambe wakamwanzishia songombingo la nguvu
na kufikia kumvua nguo hadharani na simu ikakutwa kwenye nguo yake ya
ndani,” shuhuda wetu alisema.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, hadi kufikia kupatikana
kwa simu hiyo, mrembo huyo alikuwa hoi kutokana na vurugu aliyofanyiwa
na wapambe wa Hashim ambao walipoipata simu walimvisha nguo pamoja na
wigi lake lililokuwa limemvuka.
0 comments:
Chapisha Maoni