Wakati alipoolewa kuwa mke wa pili kwa mahari ya ng’ombe wanane,
Katarina Mturi (22) alisindikizwa kwa ngoma na tamaduni za Kabila la
Kikurya, wala hakuamini kama kuna siku ataichukia ndoa hiyo.
Inawezekana hakuamini hivyo kwa kuwa mume wake
Matata Makali (siyo jina halisi), ambaye alionekana mwenye upendo na
kujali, pengine ni kwa sababu ya mapenzi mapya ya binti mdogo.
Katarina alikuwa ameolewa mara ya pili akitoka kwa
mume wake wa kwanza aliyedai hakuwa na hata chembe ya upendo ndipo kwa
kushauriana, familia yake ilimrudishia mahari mwanaume huyo na ndoa
kuvunjika.
Mwanamke huyo anasema kuwa alikaa nyumbani kwao kwa muda, ndipo akajitokeza Matata(45), akiamini kuwa sasa amepata mume mwema.
Hata hivyo, hali ilikuwa kinyume, kwani leo
Katarina ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Chinato, kijijini Bisarara,
Kata ya Sedeco katika Wilaya ya Serengeti iliyopo Mkoa wa Mara, amekuwa
miongoni mwa wanawake wanaosimulia ukatili wa kijinsia katika ndoa.
Kutokana na yaliyomkuta, anaona kuwa ndoa siyo tena hitaji lake muhimu
maishani.
Kwa nini?
Pamoja na mateso, kipigo alichokuwa akipata,
alijitahidi kuvumilia familia yake ikimtia moyo na kumweleza kuwa ndoa
ndivyo zilivyo.
Lakini Katarina anasema hatosahau tukio la saa
2:30 usiku, Januari 8 mwaka huu, ambapo mumewe huyo mpya alimfanyia
ukatili bila kuwa na chembe ya huruma.
Katarina anaeleza kwamba hofu yake sasa ni ukatili kumwachia ulemavu.
“Katika hali ambayo mpaka leo sijaielewa, nilikuwa
ndani na
wanangu wawili, mkubwa na huyu mdogo mume wangu aliingia ndani akaniamuru niswage ng’ombe usiku huo kwenda ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa malisho. Nilikakataa, kwa sababu ilikuwa ni usiku. Nilimweleza kuwa kisheria haikubaliki kuchungia mifugo ndani ya Hifadhi ya Taifa, tena kuna wanyama wakali na mimi ni mwanamke nitafanyaje?,” anasimulia.

Katarina anaongeza akionyesha maeneo aliyoumizwa: “Maneno hayo yakamkasirisha na kilichotokea ndiyo kama unavyoona.”
0 comments:
Chapisha Maoni