Tarehe 09.01.2014 majira ya saa 06:00hrs huko katika kijiji cha ilenge, kata ya kyimo, tarafa ya ukukwe wilaya ya rungwe mkoa wa mbeya.
Magreth Ijumba, miaka 55, kyusa, mkulima, mkazi wa kijiji cha ilenge aliuawa akiwa nyumbani kwake kwa kupigwa jiwe kichwani na mtu/watu wasiofahamika kisha kutupwa katika shamba lake la migomba umbali wa mita 69 kutoka nyumbani kwake.
Mbinu ni kuvunja mlango wa nyumba ya mhanga ambaye anaishi peke yake kuingia ndani na kumuua kwa kutumia jiwe.
Aidha watu hao pia walikwenda mtaa wa pili na walimshambulia kisa ephraim, miaka 50, kyusa, mkulima, mkazi wa kijiji cha ilenge kwa kutumia jiwe kichwani na amelazwa hospitali ya misheni igogwe.
Chanzo ni imani za kishirikina. Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed. Z. Msangi anatoa wito jamii kuacha kuamini imani potofu za kishirikina kwani zina madhara makubwa katika jamii.
Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mtu/watu waliohusika na tukio hili azitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.



0 comments:
Chapisha Maoni