Jumatatu, Oktoba 14, 2013

WAGANGA KUTIBU GONJWA LA JOKATE?

BAADA ya Mtangazaji wa Channel O Bongo, Jokate Mwegelo kuripotiwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu, waganga wa kienyeji wamejitokeza kutaka kumsaidia ili aondokane na ugonjwa huo.
Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, baadhi ya waganga hao walisema kuwa ugonjwa unaomtesa Jokate wanaweza kuutibu kwani wamewatibu watu wengi na wamepona kabisa.
“Mimi siyo daktari ila ni mganga wa kienyeji nina uwezo wa kutibu pumu. Naomba unikutanishe na Jokate ili nimsaidie kwani nimeshawatibu watu wengi na wamepona,” alisema mmoja wa waganga hao aliyejitambulisha kwa jina la Juma.

0 comments:

Chapisha Maoni